Ruka hadi kwenye maudhui makuu

homa ya mapafu kwa watoto

HOMA YA MAPAFU KWA WATOTO PNEUMONIA FOR KIDS
Uhakika med 2 weeks ago
Homa ya mapafu ni aina ya maambukizi yanayoathiri mapafu. Ni ugonjwa ambao unaua watoto wengi hasa katika nchi zinazoendelea duniani. Inakadiriwa kwamba watoto karibu milioni 1.6 walio chini ya miaka 5 wanakufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu. Kutokana na vifo vingi vinavyotokana na homa ya mapafu tarehe 12 ya mwezi wa Novemba kila mwaka imefanywa kuwa siku rasmi ya homa ya mapafu duniani, ambapo nembo ya siku hiyo ni nguo za rangi ya bluu.




Muundo wa Mapafu


Mapafu yanajumuisha mirija mikubwa ya hewa (bronchi) ambayo hugawanyika kufanya mirija midogo zaidi ya hewa (bronchioles), ambayo nayo hutengeneza vifuko vidogo vidogo ya hewa (alveoli). Vifuko hivi vidogo vya hewa (alveoli) vina mishipa ya kupitisha damu (capillaries) ambayo husaidia kuchuja na kusafirisha hewa safi ya oksijeni tunayovuta kuingia kwenye damu na hewa chafu ya ukaa (kaboni dioksidi) kuondolewa kwenye damu na kuingizwa kwenye mapafu tayari kwa kutolewa nje ya mwili.

Kwa kawaida vifuko hivi vidogo hujaa hewa muda wote tayari kwa kusafirishwa. Inapotokea mtu akapata homa ya mapafu, vifuko hivi hujaa maji au usaha hivyo kuathiri upitishaji wa hewa safi kwenye damu na kusababisha tatizo la kupumua.



   


Homa ya mapafu husababishwa na nini?

Kuna aina kadhaa ya vimelea ambao vinaweza kusababisha maambukizi ya mapafu. Vimelea hivi hujumuisha bakteria, virusi, parasite na fangasi.Vimelea hawa hushambulia mwili wa binadamu kulingana na umri na kinga ya mwili. Kwa mfano, bakteria wanaosababisha homa ya mapafu kwa watoto wachanga ni tofauti na wale wanaosababisha ugonjwa huo kwa watoto wakubwa.
Baadhi ya vimelea wa bakteria wanaoshambulia watoto ni pamoja na Streptococcus pneumoniae ambao ni aina ya bakteria wanaoongoza kusababisha homa ya mapafu kwa watoto. Wapo pia Haemophilus influenzae aina b (Hib) ambao ni aina ya pili ya bacteria walio maarufu zaidi kwa kusababisha ugonjwa wa homa mapafu kwa watoto. Staphylococcus aureus ni aina nyingine ya bacteria ambao hushambulia zaidi watoto wachanga. Kuna pia Group B streptococci ambao pia hushambulia zaidi watoto wachanga.
Kwa upande wa virusi, virusi wa aina ya Respiratory syncytial virus ndiyo wanaoongoza kwa kusababisha homa ya mapafu kwa watoto.
Aidha, vimelea wa Pneumocystis jiroveci ambao kwa sasa huwekwa kwenye kundi la parasite ni maarufu zaidi miongoni mwa parasite wanaosababisha homa ya mapafu kwa watoto wenye upungufu wa kinga mwilini hususani watoto wenye VVU.
Aina nyingine za bakteria ambao hushambulia zaidi watoto wakubwa ni pamoja na Mycoplasma pneumonia naChlamydia pneumonia.




Jinsi Homa ya Mapafu inavyoenezwa


Kuna namna nyingi za kuenea kwa homa ya mapafu. Kwa kawaida, virusi na bacteria hupatikana katika sehemu ya juu ya mfumo wa njia ya upumuaji (upper respiratory tract). Inapotokea kinga ya mwili ya mtoto imeshuka kwa sababu yeyote ile, vimelea hivi huweza kusambaa na kufika mpaka sehemu ya chini ya mfumo wa njia ya upumuaji (lower respiratory tract) na hatimaye kushambulia mapafu. Hali kadhalika, vimelea hawa wanaweza kuenea kwa njia ya damu kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kabla ya kuzaliwa yaani kipindi cha mimba.

Dalili za ugonjwa wa homa ya mapafu



Dalili za vichomi au homa ya mapafu kwa watoto hutegemea na umri wa mtoto. Kwa watoto wadogo, dalili za awali zinaweza kuwa homa kali pamoja na mtoto kuhangaika na kunyong’onyea. Watoto wanaozaliwa wakiwa na uambukizi wa bacteria aina ya Streptococcus kundi B wanaweza kuwa na homa na kupumua kwa shida. Wakati mwingine mtoto anaweza kuwa na dalili ambazo si maalum (no-specific symptoms) kama vile kuhangaika na kushindwa kunyonya au kula vizuri bila kuwa na dalili yeyote ya kushindwa kupumua. Hali hii inaweza kutokea kwa mtoto wa umri wowote ule. Dalili za kawaida za homa ya mapafu ambazo huwapata karibu watoto wote wanaoathirika na ugonjwa huu ni pamoja na:
homa
Kuhisi baridi
kikohozi
Kupumua kwa haraka kuliko kawaida
kutoa sauti isiyo ya kawaida wakati wa kupumua
Mbavu za mtoto kuingia ndani wakati wa kupumua
maumivu ya tumbo
kupoteza hamu ya kucheza
kupoteza hamu ya kula na kushindwa kunyonya
Mtoto kubadilika rangi na kuwa na rangi bluu katika midomo na kucha
Hata hivyo, si lazima dalili zote hizi ziwepo kwa kila mtoto. Baadhi ya watoto huonesha kupumua kwa haraka kama dalili pekee ya homa ya mapafu. Iwapo vimelea vimeshambulia sehemu za chini ya mapafu karibu ya tumbo, sehemu ijulikanayo kama kiwambo au diaphragm, mtoto anaweza asioneshe hali yeyote ya kushindwa kupumua ingawa anaweza kuwa na homa na kujihisi maumivu makali ya tumbo, vichomi na pia kutapika.
Watoto wachanga wanaweza kushindwa kunyonya, na pia kupoteza fahamu na kupata degedege.




Vihatarishi vya homa ya mapafu (risk factors)


Katika hali ya kawaida kinga ya mtoto mwenye afya njema humlinda asishambuliwe na vimelea vinavyosababisha magonjwa mbalimbali. Hali huwa ni tofauti pale ambapo kinga ya mtoto ni ndogo au dhaifu, kwa vile mfumo mzima wa ulinzi huathirika na hivyo basi inakuwa ni rahisi kwa mtoto kupata homa ya mapafu.
Mfumo wa kinga wa mtoto unaweza kuwa dhaifu kwa ukosefu wa lishe bora hasa kwa watoto wachanga ambao hawanyonyeshwi ipasavyo. Aidha uwepo wa magonjwa mengine, kwa mfano, maambukizi ya VVU, saratani na ugonjwa wa Surua hupelekea kinga ya mwili kuwa dhaifu.
Lakini vile vile kuna mazingira yanayoweza kusababisha mtoto kuwa katika hatari ya kupata homa ya mapafu mfano moshi wa sigara, au moshi ndani ya nyumba unaosababishwa na kupikia kuni au mkaa. Vilevile msongamano ndani ya nyumba kutokana na watu kuwa wengi sehemu moja nayo huweza kusababisha watoto kupata homa ya mapafu.




Uchunguzi na Vipimo


Daktari humchunguza mtoto mgonjwa kwa kusikiliza dalili za ugonjwa kutoka kwa mzazi/mlezi wa mtoto, kuchunguza viashiria vya ugonjwa huu na kisha kumpima mtoto kwa kutumia kifaa kinachosaidia kusikia sauti mbalimbali katika mfumo wa hewa wa mgonjwa kiitwacho stethoscope.
Ili kujiridhisha na kuwa na uhakika wa tatizo hili, vipimo vifuatavyo vinaweza kufanywa kulingana na mazingira na upatikanaji wake. Vipimo hivyo ni pamoja na X-ray ya kifua, au CT-scan ya kifua, pamoja na damu ili kuchunguza madhara yaliyoletwa na homa hii ya mapafu.
Faida ya kipimo cha CT-scan ni ule uwezo wake wa kutofautisha aina tofauti za homa ya mapafu na aina ijulikanayo kama Atypical pneumonia ambayo si rahisi kuonekana kwa kutumia X-ray ya kawaida ya kifua. X-ray ya kifua na CT-scan ya kifua kwa pamoja vina uwezo wa kuonesha tatizo hata pale ambapo daktari ameshindwa kusikia sauti maalum kwa kutumia kifaa chake cha stethoscope.




Matibabu
Maamuzi ya Matibabu kwa watoto wenye homa ya mapafu hutegemea aina ya vimelea, umri na hali ya mtoto. Mara nyingi antibiotics ndizo hutumika katika kutibu homa ya mapafu inayosababishwa na maambukizi ya bakteria. Kwa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi, antibiotics hazina uwezo wowote wa kutibu. Ieleweke kuwa ni tabibu anayeweza kufahamu kama mtoto wako anahitaji antibiotics au dawa za aina nyingine, kwahiyo ni muhimu kwa mzazi ama mlezi kumpeleka mtoto hospitalini haraka pindi mtoto anapoonesha dalili za ugonjwa huu badala ya kuamua kumpa dawa bila kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.




Namna ya kuzuia Homa ya mapafu
Homa ya mapafu inaweza kuzuiwa kwa chanjo, lishe bora na ya kutosha na mtoto kuishi katika mazingira yenye hewa safi.
Kuzuia homa ya mapafu kwa watoto ni sehemu muhimu ya mkakati wa Taifa wa kupunguza vifo vya watoto. Chanjo dhidi ya Hib, pneumococcus, surua na kifaduro ni njia mojawapo ya kuzuia homa ya mapafu.
Lishe ya kutosha ni muhimu kwa kuboresha kinga ya mwili ya mtoto ambapo inashauriwa mama kunyonyesha mtoto bila kuchanganya na kitu chochote walau kwa miezi sita ya mwanzo ya maisha yake.
Kuhimiza usafi katika makazi kama kutotumia jiko la mkaa au kuni ndani ya nyumba na uvutaji wa sigara ni jambo linaloshauriwa pia. Hii inasaidia kupunguza idadi ya watoto kupata homa ya mapafu. Kwa watoto wenye VVU, matumizi ya dawa ya cotrimoxazole kila siku husaidia kupunguza uwezekano wa kupata homa ya mapafu.



Utafiti umeonyesha kwamba kinga na tiba sahihi ya homa ya mapafu inaweza kuzuia vifo milioni moja kwa watoto duniani kila mwaka. Hivyo ni wajibu wetu sote kushirikiana kupambana na ugonjwa huu wa homa ya mapafu



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

PAKUA PICHA ZENYE UJUMBE WA MAPENZI HAPA

KWA WALE WAPENZI WA PICHA ZENYE UJUMBE WA MAPENZI BASI HIZI HAPA Uhakika media 

Dawa 8 zinazo tibu kipanda uso kwa haraka

Uhakika media Dawa za asili 8 zinazotibu kipanda uso kwa haraka Dawa za asili 8 zinazotibu kipanda uso kwa haraka   Kipanda uso ni ugonjwa gani?   Kipanda uso ni maumivu ya kichwa ambapo kichwa kinagonga kweli kweli na mara nyingine inaweza kuwa sehemu ya mbele au upande mmoja wa kichwa ndiyo unapatwa na maumivu haya.   Maumivu haya yanaweza kubaki kwa saa 4 mpaka saa 72. Vile vile dalili za ugonjwa huu zinatofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine.   Dalili za Kipanda Uso:   Unaweza kupata baadhi ya ishara za ugonjwa huu kama vile; 1. Kujisikia uvivu, 2. Kutapika, 3. Mauzauza, 4. Kusikia kelele sikioni nk. Wakati mwingine kabla ya kipanda uso watu wengine wanaweza kupatwa na miwasho, shingo nzito, kupiga miayo, kusikia njaa nk Sababu za kutokea kipanda uso mara nyingi ni pamoja na: 1. Mfadhaiko wa akili (stress) 2. Kelele nyingi kuzidi 3. Kuluka kula mlo 4. Pombe 5. Sigara 6. Shinikizo la chi

SIMULIZI NZURI NA ZA KUSISIMUA sehemu ya 1

Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 1 Uhakika media SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA Mwandishi: SEID BIN SALIM SEHEMU YA KWANZA Mwaka mmoja ukiwa umepita tokea binti mwenye umri wa miaka 24 lucky ajiunge na chuo kikuu cha dar es salam UNIVERSITY OF DAR ES SALAM. Marafiki zake aliokuwa anakaa nao chumba kimoja katika hostel waliojulikana kwa majina ya Mariam, Tunu, na amina. Asubuhi na mapema ya wiki end waliamua kumkalisha chini rafiki yao huyo kwa ajili ya kuongea nae mambo flan, kutokana na jinsi walivyokuwa wanaishi nae katika hali ya unyonge na kuonekana hapend kushirikiana na mtu yoyote kimasomo hd starehe za hapa na pale. waliishi nae kama sio mwenzao, walipoitaji ushirikiano wake hakuitaji kuwa nao, muda mwingine walimshuhudia akikaa kiupweke hadi kutoa machozi kwa muonekano wa kuwaza mambo mazito aliyonayo moyoni mwake, walimuonea huruma hasa kwa sababu wao ni watu waongeaji, walimkalia vikao vya kimya kimya walipopata nafasi ya kipeke ya

NJIA 10 ZA KUTONGOZA KWA MACHO ZINAZO FANYA KAZI

Njia 10 za Kutongoza Kwa Macho Ambazo Hufanya Kazi Uhakika media   Je wataka kujifunza jinsi ya kutumia macho yako kupitisha ujumbe wa kuonyesha umevutiwa na mtu fulani? Kutumia macho kama mbinu ya kutongoza ni njia rahisi ya kupitisha ujumbe kutoka kwako hadi kwa yule unayemzimia kwa urahisi bila hata kutamka neno lolote. Mwanzo mchezo wa kutumia macho kama mbinu ya kutongoza huwa ina raha yake kiasi flani. Uzuri wa kutumia mbinu hii ni kuwa ni rahisi kufahamu kiwango gani mtu amevutiwa nawe bila kuwauliza kuwatoa out. Pili ni kuwa uzuri wa kutumia mbinu hii ni kuwa unamjulisha unayemzimia na mapema ya kuwa umewavutia hivyo kujitayarisha na mapema iwapo atakubali kufanya maongezi na wewe. So ni mbinu zipi hizo unazoweza kutumia kumvutia unayempenda bila kuonekana kama fala? Njia za kutongoza kwa kutumia macho Utafanya nini iwapo umemuona yule aliyekupendeza katika mkahawa ama katika party ulioalikwa na marafiki zako? Kama hujui la kufanya basi tumia macho yako kumtongoza ili

Hatua za kufuata wakati wa tendo la ndoa

USIJE UMBUKA, SOMA HATUA ZA KUFUATA WAKATI WA KUFANYA MAPENZI....! Uhakika media Wapnzi na wanandoa wengi hivi leo wanapoingia kitandani tayari kwa kuianza safari ya kupeana haki zao za msingi hushindwa kufurahia tendo na hasa hali hii hujitokezwa kwa wanawake kwani mwanaume huwa na haraka iliyopitiliza!   Mwanaume atamkumbatia na kumbusu mwanamke kwa muda mfupi na kabla hata hamasa ya mapenzi ya mwanamke ahaijashika hatama, atamwingilia na ndani ya dakika sekunde ama dakika zisizozidi 3, mwanamme hufika mshindo. Katika hali ya kusikitisha baada ya mwanaume kujitosheleza hujongea pembeni bila kujali mwenza wake hajafika mwisho wa safari hali inayosababisha mwanamke kupoteza hamu ya tendo endapo endapo tabia hiyo ya mwanaume itaendelea. Kunahatua nne muhimu ambazo wapendanao wakizishika na kuzitekeleza ipasavyo basi watafanikiwa kujitosheleza kila wanapokutana na kwa hakika watakuwa miongoni mwa watu wachache wanaofurahia faragha kila wakutanapo! Hatua ya kwanza ni kus

Dawa mbadala ya kutibu uke mkubwa au ulio legea

DAWA MBADALA ZINAZOTUMIKA KUREJESHA UKE MKUBWA AU ULIOLEGEA Jinsi gani ya kukaza uke au ni namna gani kufanya uke uwe mdogo tena ni mada au somo lisilopendwa kuzungumzwa na watu wengi. Ikiwa wewe ni mmoja wa waathirika na tatizo hili basi tumia muda wa kutosha kusoma makala hii sasa hivi, irudie mara nyingi mpaka umeielewa. Kwenye makala hii nakwenda kukuonyesha baadhi ya mbinu za jinsi gani ya kurudishia tena uke mkubwa au uliolegea na kuwa mdogo tena ukiwa nyumbani bila kuhitaji kutumia matibabu mengine ya bei kubwa. KINACHOSABABISHA UKE KULEGEA Uke kulegea au kuwa mkubwa zaidi unaweza kutokea kutokana na sababu nyingi. Kumbuka pia kushiriki tendo la ndoa mara chache siyo suluhisho la kuwa na uke mdogo. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa kuwa na uke mkubwa na kushiriki tendo la ndoa mara nyingi. Pia hakuna uhusiano wa umri na ukubwa wa uke. Wapo wamama watu wazima wana uke mdogo pia kuna wasichana wadogo kabisa wana uke mkubwa kupitiliza. Watu wengine huamini kuwa mwanamke mw

Madawa mbadala 6 ya kutibu ganzi ya mikono na miguu

Dawa mbadala 6 zinazotibu ganzi mikononi na miguuni Published by fadhili on 17/11/2017 DAWA MBADALA 6 ZINAZOTIBU GANZI MIKONONI NA MIGUUNI Ganzi mikononi na miguuni inamaanisha kukosekana kwa fahamu katika sehemu hizo. Hisia ndiyo inakosekana sababu kunakuwa hakuna damu na neva zinakosa mawasiliano rya moja kwa moja na ubongo. Ni jambo la kawaida linalowapata watu wengi sana miaka ya hivi karibuni. Kinachosababisha ganzi mwilini ni pamoja na: 1. Shinikizo la muda mrefu kwenye miguu na mikono 2. Kuwa karibu na vitu vyenye baridi sana kwa kipindi kirefu 3. Mabadiliko ya muda mfupi kwenye neva 4. Ajali kwenye neva 5. Kunywa pombe kupita kiasi 6. Uvutaji wa sigara na bangi 7. Uchovu sugu 8. Kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara 9. Ukosefu wa vitamini B12 na Magnesiamu 10. Ugonjwa wa kisukari nk Kwa kawaida ganzi inayotokea kwa dakika kadhaa na kupotea huwa haina shida yoyote lakini onana na daktari mapema ikiwa inakutokea mara kwa mara na pia ikiwa inakutok

VIDEO: Mbwembwe za Joti aingia uwanjani kisa Samatta nusra akamatwe na polisi' refa amtoa

VIDEO: Mbwembe za Joti aingia uwanjani kisa Samatta nusra abebwe na polisi, refa amtoa Uhakika media 1  · 12 hours ago Joti ambae ni msemaji wa team Samatta leo ameonyesha vituko vya aina yake ambapo imepelekea baadhi ya mashabiki kuachwa midomo wazi kwa kitendo cha kuingia uwanjani wakati mpira uneendelea baada ya Mbwana Samatta kufanyiwa madhambia kwenye eneo la hatari  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Jinsi ya kurudisha hisia za mapenzi zilizo potea

Jinsi ya kurudisha hisia za mapenzi zilizopotea uhakika media 2  · 9 hours ago Tunaishi kwenye ulimwengu unaoenda kasi sana kiasi kwamba usipokuwa makini, unaweza kujikuta ukimpoteza mtu uliyempenda sana maishani kwa sababu tu ya kutojua namna ya kwenda naye sawa. Inafahamika kwamba mapenzi ni hisia lakini ni wachache wanaoweza kueleza jinsi ya kufanya hisia za mapenzi ziendelee kuwa hai. Siku hizi ndoa nyingi zinaendelea kuwepo kwa sababu ya kudra tu, unakuta mume na mke wanaishi kwa sababu ya mazoea tu lakini si kwa sababu ya mapenzi! Wengine wanakwambia kabisa, ‘mapenzi yalikuwa wakati tunaanzana’! Wanaishi tu ilimradi siku zinaenda, ilimradi wanawalea watoto lakini si kwa sababu ya upendo kati yao. Wengine wanafikia hatua hata ya kulala mzungu wa nne au kutengana vyumba kabisa! Au kwenda kulala vyumba vya watoto, watu haohao Kwa nje mnawaona kama wanapendana lakini kumbe ndani kuna ufa mkubwa kati yao, hakuna tena mapenzi kati yao. Cha ajabu, utakuta watu hawahawa am

MBINU 10 ZA KUONGEZA MBEGU ZA KIUME

Mbinu 10 za kuoongeza mbegu za kiume (sperm count) Mwanaume mwenye uwezo wa kuzalisha anahitaji kuwa na mbegu zisizopungua milioni 20, chochote chini ya hapa kinaweza kuwa sababu ya kutokutungisha ujauzito. Ikitokea umegundulika kuwa na mbegu chache, ni nyepesi sana na hazina nguvu za kukimbia vya kutosha basi makala hii itakupa maelezo juu ya mbinu 10 zinazoweza kukusaidia kuongeza uwingi wa mbegu zako bila gharama yoyote. Visababishi vya mbegu kuwa chache: Kuna vitu vingi vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume, kwa bahati nzuri vingi ya vitu hivyo tunao uwezo wa kuvidhibiti kwa kupunguza matumizi yake. Vitu hivyo ni pamoja na: • Vifaa vya kieletroniki – Tafiti zimeonyesha vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa wingi na ubora wa mbegu kwa wanaume wengi miaka ya sasa kwani mionzi yake hupelekea joto lisilohitajika katika mifuko ya mbegu za kiume. Vifaa hivi ni pamoja na simu na Kompyuta. Unashauriwa kutokuweka