Polisi Mwanza yawaonya wanaotumia vibaya mitandao
Uhakika media / 15 hours ago
Naibu Kamishina Ahmed Msangi.
JESHI la Polisi mkoani Mwanza limewaonya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaoitumia vibaya kwa kufanya uhalifu ikiwemo kuhamasisha maandamano haramu.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Naibu Kamishina Ahmed Msangi ametoa onyo hilo wakati akizungumza na askari waliokuwa kwenye mazoezi mbalimbali yaliyofanyika katika uwanja wa polisi Mabatini jijini Mwanza.
RPC Ahmed Msangi alisema; "Kuna watu wanapeana vihabari vya kwenye mitandao ya kijamii wafanye uhalifu na uhalifu wenyewe ni wa kufanya maandamano au mkutano usiokuwa na taarifa na kiukweli imepigwa marufuku"
Aidha, RPC Msangi amewataka Polisi kufanya uchunguzi ili kuwabaini wanaoshinikiza hayo na kisha kuwahoji na kujua nia yao ya kutaka kufanya hivyo ni ipi.
Baadhi ya askari walioshiriki mazoezi hayo wameeleza kwamba yanawasaidia kuwa imara wakati wote na hivyo kutimiza vema majukumu yao.
Maoni
Chapisha Maoni