Uhakika media 2 · 1 hour ago
FAMILIA ya Nguza Viking Mbangu, ‘Babu Seya’, imefunguka kuwa baada ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (AfCHPR) kukubali hoja zao tatu kati ya nane za ukiukwaji wa haki za binadamu katika hukumu ya kifungo cha maisha kwa mwanamuziki Nguza na mtoto wake, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ ambao walitiwa hatiani kwa makosa ya ubakaji na ulawiti, kwa sasa hawawezi kuongea chochote hawawezi kwanza wawasiliane na wakili wao.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Mbangu Nguza ambaye ni msemaji wa familia alisema kuwa, kwanza anashukuru kwa hoja zao tatu kukubaliwa na mahakama hiyo na wanamshukuru Mungu kwa hilo.
“Kwa kweli tunamshukuru sana Mungu kwa kuwa anatenda kama maombi yetu yalivyo, lakini kuhusu kudai fidia hayo ni mpaka tukae kifamilia na wakili wetu ambaye yupo Arusha,” alisema Mbangu ambaye ni mmoja wa watoto wa Babu Seya.
Akisoma hukumu katika kesi hiyo, iliyochukua dakika 55, mwishoni mwa wiki iliyopita, Jaji Gerard Niyungeko kwa niaba ya majaji wenzake saba wa mahakama hiyo, alisema kuwa, kutokana na hoja nane zilizowasilishwa mahakamani hapo katika shauri hilo namba 006/2015, ilijiridhisha kwamba hoja tano hazikuwa na ukiukwaji wa haki hasa kutokana na maelezo ya walalamikaji.
Akizungumzia hoja ya kulipwa fidia kutokana na gharama za kesi hiyo na madai mengine, Jaji Niyungeko alisema kuwa, mahakama ilitoa mwezi mmoja kwa walalamikaji kuwasilisha mahakamani hapo madai yao ya fidia kama watahitaji na kutoa muda kama huo kwa serikali kuyajibu kabla ya kutoa uamuzi juu ya madai hayo ya fidia.
Jaji Niyungeko ambaye ni Raia wa Burundi alisema kuwa, jopo hilo la majaji lilijiridhisha bila shaka kwamba, hoja tatu zilizowasilishwa na walalamikaji zilikuwa na mashiko.
Hoja hizo ni ile iliyowasilishwa na walalamikaji kwamba mtuhumiwa wa kwanza, Nguza wakati wa mwenendo wa kesi hiyo, alieleza kuwa hana nguvu za kiume hivyo asingeweza kufanya vitendo vya ubakaji na alitaka mahakama kutoa agizo la kupimwa na madaktari hatua ambayo haikukubalika.
Jaji Niyungeko alisema kuwa, hoja nyingine ambayo ilibainika kuwa na mashiko ni kuwa walalamikaji hawakupata maelezo ya mashahidi na walikubaliana na hoja kuwa watuhumiwa ambao sasa wapo huru kutokana na msamaha wa rais, hawakupata fursa ya kuwauliza maswali waliotoa ushahidi ili kuthibitisha makosa, jambo ambalo ni kosa kisheria.
Akizungumza baada ya uamuzi huo, wakili wao, Donald Deya alisema kuwa, aliridhishwa na anasubiri nakala ya hukumu ili kutekeleza maagizo ya mahakama baada ya kushauriana na wateja wake.
Babu Seya na wanaye watatu, Oktoba 16, 2003 walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar na kusomewa jumla ya mashtaka 21 ambapo Juni 25, 2004 walihukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela.
Ka nyakati tofauti walikataa rufaa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa ambako huko kote waligonga mwamba kabla ya kuachiwa kwa msamaha wa Rais John Pombe Magufuli Desemba, mwaka jana.

Maoni
Chapisha Maoni