JPM: Maaskofu hamasisheni ujenzi wa viwanda wakati wa mahubiri
Uhakika media / 17 hours ago
Rais Dk. John Magufuli
RAIS Dk. John Magufuli amewataka maaskofu badala ya kuhubiri mambo mengine, wahubiri kuhusu ujenzi wa viwanda vya dawa nchini ili Tanzania isinunue dawa nje ya nchi.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo (Machi 26, 2018) katika hafla fupi ya ugawaji wa magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), kwa ajili ya kusambaza dawa maeneo mbalimbali nchini inayofanyika eneo la Keko, jijini Dar es Salaam.
Amesema kununua dawa nje ya nchi kunasababisha nchi kupoteza sh. 500 bilioni. “Asilimia 94 ya dawa zinanunuliwa nje ya nchi, ni asilimia sita tu ya dawa zinanunuliwa ndani,” amesema.
Dk. Rais Magufuli amewapongeza MSD kwa kufanya kazi nzuri na ya kizalendo. Amesema kupatikana kwa magari hayo kumeifanya MSD kuwa na magari 213 kutoka magari 32 waliyokuwa nayo awali.
Maoni
Chapisha Maoni