Uhakika media 2 · 4 hours ago
Urusi imeiambia Uingereza kuwa lazima iwarejeshe nyumbani wanadiplomasia wake zaidi ya 50 katika mgogoro unaoendelea kuwa mbaya na nchi za Magharibi kuhusiana na shambulizi la sumu dhidi ya jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na binti yake Yulia lililotokea nchini Uingereza.
Urusi tayari imejibu hatua za Uingereza na kuwatimua wanadiplomasia 23 wa Uingereza kufuatia tukio hilo.Uingereza inasema Urusi ilihusika na shambulizi hilo, tuhuma ambazo Urusi inazikanusha.
Balozi wa Uingereza Laurie Bristow aliitwa tena jana na kuambiwa kuwa serikali yake ina mwezi mmoja kupunguza idadi ya wanadiplomasia wake nchini Urusi, ili kufikisha idadi sawa na ya ujumbe wa Urusi nchini Uingereza.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi Maria Zakharova ameliambia shirika la habari la Reuters hiyo ina maana kwamba Uingereza inapaswa kupunguza wanadiplomasia wake nchini humo kwa kuwarudisha nyumbani maafisa 50.

Maoni
Chapisha Maoni