Uhakika media 5 · 1 hour ago
Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Hassan Dalali, anaimani timu yake itatwaa ubingwa wa ligi msimu huu baada ya kuukosa kwa muda wa takribani miaka mitano.
Dalali ambaye aliwahi kufanya vizuri wakati akiwa Mwenyekiti wa Simba, amesema kikosi walichonacho hivi sasa kina morali ya juu na si kama kadhaa nyuma.
"Simba hii iko vizuri, hauwezi ukailinganisha na timu zingine katika ligi, uwezekano wa kubeba kombe upo kwa asilimia 100" alisema Dalali wakati akizungumza na kipindi cha Michezo, kupitia Radio One jana.
Aidha Dalali ametamba kwa kusema Simba ni lazima ishinde mchezo wa Jumanne dhidi ya Njombe Mji ili kuendelea kujitengenezea mazingira ya kuwa kileleni. Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Dalali ameeleza mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na kila timu kuwa na uhitaji wa alama tatu, hivyo watambana ili kupata matokeo.
Maoni
Chapisha Maoni