Uhakika media 3 · 1 hour ago
Mkuu wa mkoa wa kusini unguja mhe hassan khatib hassan amewataka vijana wa mkoa huo kutotosheka na elimu walizonazo na badala yake kujiendeleza kielimu ili kukabiliana vyema na soko la ajira.
Mhe khatib ametoa kauli hiyo dunga majenzi wakati alipokuwa akiyafunga mafunzo ya usafi wa mazingira kwa vijana wa kampuni ya asphys cleaning and security ambao wanatokana na baraza la vijana kutoka shehia 42 za wilaya ya kati.
Amesema ili vijana waweze kupiga hatua za maendeleo na kukabiliana na soko la ajira hawana budi kuwa na elimu ya kutosha itakayokidhi mahitaji hasa kwa wakati huu ambao nchi inaelekea kwenye uchumi wa kati na waviwanda.
Aidha mkuu huyo amewataka vijana hao kuzitafuta na kuzichangamkia fursa mbali mbali zilizopo ndani ya mkoa huo sambamba na kubuni miradi itakayoweza kuwaingia kipato na kuweza kujikwamua kimaisha.
Nae meneja wa kampuni hiyo ndugu yussuf abdalla abdalla amesema lengo la ufunguaji wa kampuni hiyo ni kuweza kuwasaidia kuwapatia ajira vijana waweze kujikwamua kimaisha na kuondokana na mawazo ya kutegemea ajira kutoka serikali kuu.
Katika risala yao vijana hao wamesema licha ya jitihada mbali mbali wanazozichukuwa lakini bado wanakabiliwa na changamoto zikiwemo ukosefu wa ofisi ya kudumu, upungufu wa vitendea kazi na kutokupata tenda za kutosha za kufanya kazi.
Kampuni hiyo tayari imeshasajili vijana wapatao 148 wakiwemo wanawake 81 na wanaume 67 kati ya hao 60 wamepatiwa mafunzo ya kufanya usafi wa majengo, maeneo wazi na usanifu wa bustani.
Maoni
Chapisha Maoni