Uhakika media 5 · 1 hour ago
Baada ya kuwasili jana Iringa, kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi leo kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji.
Simba wanakibarua cha mechi dhidi ya Njombe Mji FC kitakachopigwa Jumanne ya wiki ijayo Aprili 3 2018 kwenye Dimba la Sabasaba.
Simba watakuwa wanafanya mazoezi hayo bila kiungo wao, Jonas Mkude, ambaye bado hajakaa sawa baada ya kuumia kifundo cha mguu wakati wakifanya mazoezi jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo kikosi kilimjumuisha Mkude katika safari ya Iringa baada ya Daktari wa timu, Yassin Gembe, kusema hatochukua muda mrefu kupona kutokana na maumivu ya jeraha hilo kuwa dogo.
Kuna hatihati ya kiungo huyo kucheza dhidi ya Njombe kulingana na maumivu aliyoyapata kwenye kifungo hicho cha mguu wake.
Maoni
Chapisha Maoni