Uhakika media 3 · 1 hour ago
Tanzania Prisons imekuwa timu ya pili kubebeshwa virago katika Azam Sports Federation Cup baada ya kukubali kulamba mchanga kwa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ulianza kutikiswa nyavu zake mnamo dakika ya 43 kipindi cha kwanza na Shiboli ambaye aliufanya mchezo huo kwenda dakika 45 za kwanza matokeo yakiwa ni 1-0.
Kipindi cha pili JKT Tanzania walizidi kulifumania lango la wapinzani wao 'Tanzania Prisons' ambapo katika dakika ya 73, Matelema alipiga msumari wa mwisho kwa kufunga bao la pili. Mpaka Mwamuzi anapuliza kipyenga cha mwisho, Tanzania Prisons 0-1 JKT Tanzania.
Matokeo hayo yanaifanya JKT Tanzania iwe timu ya pili kutinga nusu fainali ya mashindano hayo baada ya Stand United kutoka Shinyanga kuingia hatua hiyo jana.
Mchezo mwingine utakaopigwa jioni ya leo majira ya saa moja utawakutanisha Azam FC watakaokuwa nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar.
Maoni
Chapisha Maoni