Uhakika media 3 · 1 hour ago
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria na Utumishi wa Umma na Utawala bora Haroun Ali Suleiman amewataka Viongozi wa Taasisi kufanya kazi kwa kuzingatia Maadili na Utawala bora ili kusaidia kupunguza tatizo la Rushwa Nchini.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa maadili ,Rushwa na Uendeshaji wa Mashtaka Mjini Zanzibar Waziri Harouna Amesema wakati umefika kwa Viongozi wa taasisi kufuatilia vitendo vya rushwa vinavyofanywa na Baadhi ya wafanya kazi katika Ofisi zao ili kuthibiti tatizo la Rushwa.
Amesema suala la Udhibiti wa Rushwa linahitaji mashirikiano kati ya Viongozi na jamii ili kuendeleza dhana ya utawala bora Nchini.
Waziri Haroun amesema kuendelea kuwepo kwa kesi na Vitendo vya Rushwa kunasababisha athari mbali mbali kwa wananchi ikiwemo wananchi kukosa kunufaika na haki zao za msingi hususan katika Miradi ya maendeleo.
Aidha ametowa wito kwa wasimamizi wa sheria kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na Vitendo vya Rushwa hususani katika ngazi za maamuzi ili wananchi waweze kunufaika na haki zao.
Akizungumzia lengo la Mkutano huo Mkurugenzi Mkuuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar ZAECA Mussa Haji Ali amesema lengo ni kutoa elimu kwa Tasisi na wananchi juu ya utawala bora, Rushwa na uendeshaji wa Mashtaka ili wahusika waweze kufanya kazi kwa maadili na sheria.
Amesema kumejitokeza tatizo la uelewa mdogo kwa jamii na baadhi ya watendaji juu ya kuendelesha kesi na masuala ya rushwa na kusababisha wananchi kushindwa kufuatilia kesi zao kwa kufuata sheria.
Amesema katika kuhakikisha wananchi wanananufaika na haki zao za msingi ZAECA itaendelea kutoa elimu kwa wananchi na taasisi mbali mbali ili kupunguza tatizo la uhaba wa elimu katika Masula ya Rushwa na mashtaka hususan katika Utoaji wa Ushahidi.
Wakati huo huo ZAECCA imezingua namba ya Simu ya huduma kwa wateja ili kuwawezesha wananchi kuripoti vitendo vya rushwa vinavyojitokeza katika jamiii kupitia namba 113.
Mkutano huo wa siku moja Ulioandaliwa na ZAECCA umewashirikiswa watadau Tasisi mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ambapo umejadili Majukumu ya Mkurugenzi wa Mashtaka ,Mkakati wa Kuzuia Rushwa na Mgongano wa kimaslahi katika utumishi juu ya kuimarisha utawala bora.
Maoni
Chapisha Maoni