MIGUNA ATIMULIWA TENA KUTOKA KENYA:
Uhakika media
Mwanasiasa wa upinzani atimuliwa tena kutoka Kenya na kupelekwa Dubai
Dakika 53 zilizopita
Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Mshirikishe mwenzako
Haki EPA
Bw Miguna alizuiliwa Jumatatu akijaribu kurejea Kenya uwanja wa JKIA
Mwanasiasa wa upinzani Kenya aliyeidhinisha kiapo cha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa 'Rais wa Wananchi' Januari Miguna Miguna ametimuliwa tena kutoka nchini humo.
Mwanasiasa huyo ametimuliwa huku mzozo kuhusu uraia wake ukiendelea.
Bw Miguna ameandika kwenye Facebook kwamba ameamka na kujipata yuko Dubai na kwamba anahitaji matibabu.
Amesema anafahamu kwamba kuna mpango wa kumpeleka London lakini anataka kupanda ndege ya kurejea Nairobi pekee.
Mwanasiasa huyo amesema amesindikizwa na afisa wa idara ya ujasusi.
Ruka
Mwisho
Serikali imechukua hatua hiyo licha ya kuwepo kwa maagizo ya mahakama ya kuzuia kutimuliwa kwake na ya kuitaka serikali kufanikisha kurejea kwake nchini humo.
Mawakili wa Bw Miguna wamethibitisha kwamba aliondolewa nchini humo kwa kutumia ndege ya shirika la Emirates iliyokuwa inaelekea Dubai.
Bw Miguna alikuwa amezuiliwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) tangu alipowasili Jumatatu adhuhuri.
Mwanasiasa huyo alikuwa anajaribu kurejea kutoka Canada ambako alikuwa amepelekwa baada ya kufurushwa kutoka Kenya kwa lazima mwezi Februari.
Maoni
Chapisha Maoni