Uhakika media · 1 hour ago
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, (PAC) wamestajabishwa na kitendo cha kupitisha bajeti na serikali kutoa kiasi ambacho si sahihi hali inayopelekea kurudi bungeni na kuhoji kwanini wanachindwa kuheshimu kamati hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Tathimini ya ziara ya siku mbili jijini hapa jana Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Aeshi Hilaly ambaye ni Mbunge wa Sumbawanga alisema Kamati ya bunge tulipitisha kuwa asilimia mbili ya mapato ya simu yaende kwenye miundombinu ya elimu na mwaka jana zimekusanywa shilingi Bilioni 70 lakini wametoa bilioni 10 jambo ambalo halikubaliki.
Kamati hiyo pia haikuridhishwa na ukarabati ya shule ya wasichana ya Bwiru kutokana na kuonekana kutumia kiasi kikubwa cha pesa cha zaidi ya shilingi Milioni 900 bila uhalisia.
“Tumekagua jengo la shule ya Ngaza tumeridhishwa kwani lina ubora na hili tumelichukua kwa wale ambao wamepewa mamlaka ya kusimamia Shule hiyo ya Bwiru tutakabidhi ripoti yetu na wanahusika watalifuatilia kwa mapana zaidi,” alisema Hilaly.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu (TEA) Graceline Shirima alisema serikali kwa sasa inatekeleza programu ya ukarabati wa shule kongwe 89 kwa awamu, huku shule 10 zikikarabatiwa kwa awamu ya kwanza na ikiwemo Ngaza na awamu ya pili ni shule saba.
Shirima alisema lengo la ukarabati huu ni kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia na hatimaye kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu kwa ubora na usawa unaotarajiwa.
Aidha kamati ya Bunge imesema itapeleka ombi la kuhakikisha Shilingi Milioni 200 za ukamilishaji wa jengo la Mkuu wa wilaya ya Nyamagana.
Maoni
Chapisha Maoni