Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 1 Uhakika media SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA Mwandishi: SEID BIN SALIM SEHEMU YA KWANZA Mwaka mmoja ukiwa umepita tokea binti mwenye umri wa miaka 24 lucky ajiunge na chuo kikuu cha dar es salam UNIVERSITY OF DAR ES SALAM. Marafiki zake aliokuwa anakaa nao chumba kimoja katika hostel waliojulikana kwa majina ya Mariam, Tunu, na amina. Asubuhi na mapema ya wiki end waliamua kumkalisha chini rafiki yao huyo kwa ajili ya kuongea nae mambo flan, kutokana na jinsi walivyokuwa wanaishi nae katika hali ya unyonge na kuonekana hapend kushirikiana na mtu yoyote kimasomo hd starehe za hapa na pale. waliishi nae kama sio mwenzao, walipoitaji ushirikiano wake hakuitaji kuwa nao, muda mwingine walimshuhudia akikaa kiupweke hadi kutoa machozi kwa muonekano wa kuwaza mambo mazito aliyonayo moyoni mwake, walimuonea huruma hasa kwa sababu wao ni watu waongeaji, walimkalia vikao vya kimya kimya walipopata nafasi ya kipeke ya...
Maoni
Chapisha Maoni