Uhakika media 5 · 11 minutes ago
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye anajulikana kuwa miongoni mwa wasanii wabishi linapokuja suala la maadili ya kazi zao, Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego kwa mara ya kwanza amesalimu amri ya serikali na kuwasilisha kazi yake BASATA
kukaguliwa, lakini asema sio sababu ya kumzuia kufanya atakalo.
Akizungumza na www.eatv.tv, Nay wa Mitego amesema ameamua kufanya hivyo ili kukwepa lawama za serikali, lakini bado msimamo wake ni uleule kuwa hawawezi kumpangia cha kuimba kwenye muziki wake, kwani ndio kitu ambacho mashabiki wake wanakitaka na ndio kinachomuingizia pesa.
“Nimejaribu kufuta utaratibu, nadhani hii ni ngoma ya kwanza kwa mara ya kwanza kabla haijattoka niliwatumia BASATA, nafanya muziki wangu kama nilivyokuwa naufanya nimepunguza baadhi ya vitu, siwezi nikahama kwenye muziki wangu, yaani nitaendelea kufanya muziki wangu ule ule, nimewafikishia wimbo wangu lakini si kwa ajili ya kupangiwa mashairi ya kuimba, sitaki kuanza kuzuiliwa nyimbo zangu”, amesema Nay wa Mitego.
Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wasanii kufungiwa nyimbo zake na Nay wa mitego kuwa miongoni mwa wahanga wa mara kwa mara wa tukio hilo,
Maoni
Chapisha Maoni