Uhakika media 5 · 4 minutes ago
WABUNGE wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, wamepeleka malalamiko yao kwenye ubalozi wa Ulaya nchini kuhusiana na kesi inayowakabili viongozi wa juu wa chama hicho ambao wamekuwa mahabusu toka juzi jumanne.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema amesema wameamua kufika ubalozini hapo kueleza masikitiko yao ya kucheleweshwa kufikishwa mahakamani kwa viongozi wao ambao kesi yao inapaswa kusikilizwa leo kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
Viongozi wa chama hicho ambao wanakabiliwa na kesi hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Vicent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salimu Mwalimu, Mwenyekiti wa kanda ya Nyasa na Mbunge wa Iringa Mjini, Mch Peter Msigwa pamoja na Mweka Hazini wa Bawacha na Mbunge wa Tarime Mjini, Easter Matiko.
" Tunapatwa wasiwasi na dhamana ya viongozi wetu, tunafahamu kuwepo kwa mashinikizo kutoka kwa mamlaka ya juu dhidi ya kesi hii, lakini pia kumekuwepo na hofu kwa wabunge wetu kuhusu usalama wetu na zaidi ya wabunge saba wa upinzani wana kesi mahakamani, tumekuja hapa kuongea na ubalozi wa Ulaya kuwaeleza hali ilivyo hivi sasa," amesema Lema.
Viongozi wa chama hicho waliokosa dhamana Machi 27, mwaka huu baada ya mawakili wa Serikali kuzuia dhamana hizo.
Lema amesema chama hicho kitawaomba mabalozi hao kutotoa tamko pekee bali kiende mbali zaidi huku akieleza kuwa wataomba hati ya tahadhari kwa ajili ya wabunge na viongozi wengine wa chama hicho ambao wanakabiliwa na tishio la usalama wao.

Maoni
Chapisha Maoni