Jana March 18, 2018 Rais wa MauritiusAmeenah Gurib-Fakim ametangaza kujiuzulu huku kashfa ya matumizi mabaya ya ofisi pamoja na kashfa ya matumizi mabaya fedha ikiwa inaendelea kumuandama.
Gurib-Fakim alikuwa ni rais pekee mwanamke Barani Afrika ametuhumiwa kwa kununua vitu binafsi vya kifahari vyenye thamani kubwa kwa kutumia kadi ya benki ya Taasisi ya Dunia yenye makao yake nchini Uingereza.
Gurib-Fakim alisema mapema wiki hii kwamba aliitumia kadi bila kujua, lakini alikuwa amewarudishia fedha hizo.
Hata hivyo, Rais huyo alichaguliwa kuwa rais mwaka 2015 na hapo awali alikuwa Profesa wa kemia katika kitivo cha sayansi cha Chuo Kikuu cha Mauritius.
Maoni
Chapisha Maoni