Usiku wa March 19, 2018 Rais wa Urusi Vladimir Putin ameibuka mshindi mkubwa katika uchaguzi mkuu nchini humo na ataliongoza taifa hilo kwa miaka sita.
Ushindi huo ulitarajiwa katika upigaji kura uliomalizik jumapili. Hata kabla ya kura zote kuhesabiwa tayari alikuwa amejizolea asilimia 76 ya kura kwa mjibu wa tume ya uchaguzi.
Akizungumza katika mkutano wa kutangazwa mshindi amesema ushindi wake ni matokeo ya hatua kubwa ya mafanikio aliyoyafikia katika uongozi wake.
“Sina mpango wowote wa kufanya marekebisho yoyote ya katiba, kuhusiana na uenyekiti na serikali kwa ujumla. Nilishasema awali kwamba nafikiria suala hilo. Lakini kuanzia leo naanza kufikiria kwa undani, kwa sababu nilipaswa kusubiria matokeo ya uchaguzi kwanza.Mabadiliko yote yatatangazwa yakifuatiwa na uzinduzi..” -Putin
Maoni
Chapisha Maoni