Uhakika media · 8 hours ago
UTANGULIZI
Kuwafundisha washiriki kufikiri ki- masoko na kuelewa baadhi ya mbinu za masoko kitu ambacho kitawafanya waelewwe maana ya maneno “soko na masoko” pia utafiti wa soko na kuyafanyia kazi katika biashara/miradi yao.
Soko ni nini?
Soko ni utaratibu au mtindo uliowekwa kwa mujibu wa kanuni /sheria kumwezesha mfanya biashara kuuza bidhaa zake kwa wateja/walaji. Husaidia kupanga nini uuze,nani umuuzie au jinsi gani watu wanavyoweza kujuakitu gani unauza,hivyo kukuwezesha kuzalisha kile ambacho kinahitajika katika soko sahihi.
Mafanikio katika biashara hutokana na mwonekano wa kipekee wa bidhaa au bidhaa unayozalisha kukidhi matakwa ya walaji au wateja pia, kuweza kutambua aina fulani ya watu ambao wangependa kununua bidhaa yako na kuweza kueleza bayana ni kitu gani, watu wategemee kunufaika kwa kunua bidhaa zako kati ya kundi hili la walengwa.
Kwa kifupi soko ni MTEJA Wa bidhaa na huduma uayozalisha
Soko lako ni;
Masoko ni nini?
Masoko ni shughuli yoyote ile anayofanya mfanyabiashara ili kuimarisha biashara yake.
Haitoshelezi tu kukaa kungojea oda.
Mfano wa shughuli hizo ni;
UTAFITI WA SOKO
1. Kwa nini tujifunze kuhusu soko?
a) Mahitaji (demand)
Waswahili husema ‘unaweza kumlazimisha punda aende mtoni lakini huwezi kumlazimisha anywe maji’inamaana bidhaa zako kuwa wakati soko halihitaji bidhaa zako huwezi kulazimisha bidhaa yako inunuliwe
b) Bidhaa sahihi – usijaribu kumuuzia kitana mtu mwenye kipara bali muuzie kofia
c) Kufuata mkumbo-ni vema kutofautisha bidhaa za kuuza kwa wateja
2. Unahitaji kufahamu nini kutokana na soko lako?
Maswali yafuatayo ndio yakusaidia kufanya utafiti wa soko lako
Wateja wako ni akina nani?
NB; kutafuta majibu ya maswali haya kunaitwa utafiti wa masoko
3. Jinsi ya kufanya utafiti a soko
Mbinu zifuatazo zinaeza kutumika kufanya utafiti wa soko la bidhaa au huduma unazozalisha:-
4. Jumuisho la masuala ya masoko
B-Nne katika masoko
Sifa za bidhaa

- Wateja wako ulionao kwasasa
- Wateja uaotarajia kuwapata baadae
- Wateja uliopoteza na untarajia watakurudia tena
Masoko ni nini?
Masoko ni shughuli yoyote ile anayofanya mfanyabiashara ili kuimarisha biashara yake.
Haitoshelezi tu kukaa kungojea oda.
Mfano wa shughuli hizo ni;
- Kuelewa matakwa ya wateja wa bidhaa yako
- Kupanga bei ambayo wateja watakuwa tayari kulipa na itakupa faida
- Usambazaji wa bidhaa au huduma kwa wateja wako
- Kuwavutia wateja wanaume bidhaa au huduma yako
UTAFITI WA SOKO
1. Kwa nini tujifunze kuhusu soko?
a) Mahitaji (demand)
Waswahili husema ‘unaweza kumlazimisha punda aende mtoni lakini huwezi kumlazimisha anywe maji’inamaana bidhaa zako kuwa wakati soko halihitaji bidhaa zako huwezi kulazimisha bidhaa yako inunuliwe
b) Bidhaa sahihi – usijaribu kumuuzia kitana mtu mwenye kipara bali muuzie kofia
c) Kufuata mkumbo-ni vema kutofautisha bidhaa za kuuza kwa wateja
2. Unahitaji kufahamu nini kutokana na soko lako?
Maswali yafuatayo ndio yakusaidia kufanya utafiti wa soko lako
Wateja wako ni akina nani?
- Wako wapi
- Mahitaji yao ni nini?
- Wanapendelea nini kutokana na bidhaa zako
- Ni mara ngapi na kiasi gani a wanacho nunua?
- Wana nunua wakati gani?
- Ni kiasi gani cha pesa wako tayari kutoa?
- Ni jinsi gani bidhaa zitawafikia wateja
- Washindani wako ni wapi?
- Ubora wa bidhaa zao na bei zao vikoje
NB; kutafuta majibu ya maswali haya kunaitwa utafiti wa masoko
3. Jinsi ya kufanya utafiti a soko
Mbinu zifuatazo zinaeza kutumika kufanya utafiti wa soko la bidhaa au huduma unazozalisha:-
- Kupitia Kwa wateja (kusikiliza maoni yao, kuachunguza na kuwauliza maswali).
- Kuwauliza maswali watumiaji mbali mbali wa bidhaa zako ( nini wanachohitaji na wasicho kihitaji, mapendekezo na nini kiongezwe)
- Kwa marafiki na ndugu
- Kusoma kwenye vitabu, magazeti, kusikiliza radio na kuangalia televisheni
- Kupeleka bidhaa zako katika maonesho ya biashara
- Kuangalia biashara za washindani wako: bei, ubora, tofauti za bidhaa,, kuonesha bidhaa, na huduma zinazoambatana na bidhaa zako
- Onesha sampuli ya bidhaaa au tembezasampuli ya bidhaa na waulize watu maoni juu ya bidhaa zako
4. Jumuisho la masuala ya masoko
B-Nne katika masoko
- Bidhaa
- Bei
- Banda
- Bango
a) BIDHAA- Bidhaa ni kitu chochote kinachozalishwa kwa ajili ya kuuza au kutumia.
Sifa za bidhaa
Maoni
Chapisha Maoni