Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema hatoweza kuonesha uzalendo wa soka kwa ngazi ya klabu labda mambo mengine yasiyohusiana na soka.
Akizungumza na kipindi cha Sports Hedikota kinachorushwa na Radio EFM, Manara amesema hawezi kujitolea kuishabikia Yanga hata siku moja pale inaposhiriki mashindano ya kimataifa.
Manara ameeleza kuwa aliwahi kuhamasisha timu za Tanzania kuonesha uzalendo haswa pale klabu zinaposhiriki mashindano ya kimataifa, lakini akapuuzwa na viongozi wa Yanga.
Kutokana na kuupuzwa, Haji ameweka wazi kutothubutu tena kusapoti suala hili kutokana kutoungwa mkono na baadhi ya watu.
"Haitowezekana kamwe nikaonesha uzalendo kwa klabu za Tanzania, juzi hapa niliwaomba watu tuungane tuwe kitu kimoja lakini kuna mtu mmoja kutoka upande wa pili akanijibu kwa kebehi" alisema Manara
Maoni
Chapisha Maoni