Uhakika media 5 · 31 minutes ago
MWANASOKA Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo amesema kwamba hakuna mtu hata mmoja duniani wa kumlinganisha naye kwa kipaji chake, kujituma na uadilifu wake kisoka.
Nyota huyo wa Real Madrid na mshindi wa tuzo tano Ballon d'Or hata kama mjadala wa nani zaidi kati yake Lionel Messi utaendelea, Ronaldo anaamini yeye ni namba moja katika soka.
Akizungumza katika tangazo jipya la Nike, Ronaldo alisema; “Mwanzoni nilikuwa ninaota kuwa mchezaji bora duniani.
“Rafiki zangu, walikuwa wakiniangalia kama, "unasemaje?" Nilikuwa nacheza kwa kujifurahisha, kwa utani, lakini kichwani kwangu mawazo hayo yalianza nilipokuwa Manchester, hapo ndipo nilipoanza kuamini,”.
“Siwaoni watu wangu wenye kipaji kama changu cha kujaaliwa, kujituma na maadili yangu ya soka. Hakuna mmoja wa kumlinganisha nami, hakuna mmoja atakuwa Cristiano Ronaldo. Utakuwa wewe, nitakuwa mimi,”amesema.
Ronaldo amefunga mabao 562 katika mechi 753 na taji pekee analokosa katika kabati lake ni Kombe la Dunia, ambalo akiwa na kikosi chake cha Ureno atakwenda kulipigani tena katikati ya mwaka nchini Urusi.
Maoni
Chapisha Maoni