Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Banda la kulelea vifaranga

BANDA LA KULELEA VIFARANGA
Uhakika media / 14 hours ago






Ukipenda kujenga nyumba ya vifaranga itafaa ufikirie yafuatayo:-
  • Nyumba ya vifaranga iwe karibu na nyumba yako mwenyewe ili uweze kuwakagua vifaranga wako mara kwa mara.
  • Ijengwe hatua 20 au zaidi mbali na nyumba ya kuku wakubwa, hii ni kinga mojawapo ya kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa.
  • Nyumba ya vifaranga isiruhusu ubaridi au unyevu au wanyama waharibifu kuingia. Lakini nyumba iingize hewa na mwanga wa kutosha kila wakati.
  • Nyumba iwe na eneo la kutosha ili vifaranga wapate nafasi ya kutembea kutafuta chakula na maji bila kubanana.
  • Ijengwe kwenye sehemu isiyoelekea upepo unaotoka kwenye nyumba ya kuku wakubwa. Tahadhari hii husaidia vifaranga kuepukana na magonjwa yanayoenezwa na upepo.



Eneo: Vifaranga hawahitaji eneo kubwa katika muda wa majuma 4 ya kwanza. Nafasi inayohitajiwa kwa kukadiria ni meta za eneo 1 kwa kila vifaranga 16. Kwa mfano nyumba yenye Meta 10 za mraba inatosha kulea vifaranga 160 hadi umri wa majuma 4. Vipimo vya nyumba yenye eneo kama hili inaweza kuwa na hatua 5 kwa hatua 4 au hatua 3 kwa 3.25. Utajenga kutegemea na eneo ulilonalo. Baada ya majuma 4 ya umri ongeza nafasi na uwape vifaranga eneo la kuwatosha.


Sakafu: Sakafu nzuri katika nyumba ya vifaranga ikiwezekana inafaa ijengwe na simenti iliochanganywa na zege. Ili kupunguza gharama, unaweza kutumia vifaa vya ujenzi vinavyopatikana kirahisi katika eneo lako vitumikavyo kusiriba sakafu kama udongo wa kichuguu au unaweza kulainisha kinyesi cha ng’ombe kwa maji na kusiriba eneo lote la sakafu.


Ukuta: Ingefaa kuta za nyumba za kulea vifaranga za matofali, udongo, mabati au debe. Kuta za matofari na udongo zipigwe lipu ili kurahisisha usafishaji wa nyumba au umwagiaji wa dawa. Urefu wa kuta uwe tangu meta 1.8 – 2.4 (futi 6-8). Sehemu ya kutoka chini ya meta 0.9 – 1.2 (futi 3 – 4) izibwe na ukuta wa tofali au udongo na sehemu ya juu iliyobakia yenye meta 0.9 – 1.2 (futi) 3-4) ijengwe kwa wavu wa chuma au fito.


Mbao: Nguzo za miti au mbao zilowekwe dawa ya mbao kama vile “Dudu killer” au oili chafu ili kuzuia kuoza. Ukitumia miti ni vizuri uondoe magome ambayo yanaweza kuweka vimelea na wadudu.


Madirisha: Unaweza kutumia maboksi, mikeka ya magunia, mapazia ya magunia ni rahisi na yanaweza kuwekwa kwa kupigiliwa misumari kwenye dari na upande wa chini pazia ipigiliwe misumari kwenye ubao ili ininginie.Unaweza kukunja mapazia/magunia ili uingize hewa na mwanga wa kutosha katika nyumba ya vifaranga.


Paa: Mjengo wa paa uwe unaoweza kuwapatia vifaranga hewa ya kutosha hivyo paa liwe na tundu la kutoa nje hewa yenye joto. Kwa kadri utakavyoweza, unaweza kutumia madebe, mabati, makuti au nyasi n.k. kuezeka nyumba ya vifaranga. Sehemu ya paa ikianza kuvuja iezekwe bila kuchelewa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

PAKUA PICHA ZENYE UJUMBE WA MAPENZI HAPA

KWA WALE WAPENZI WA PICHA ZENYE UJUMBE WA MAPENZI BASI HIZI HAPA Uhakika media 

SIMULIZI NZURI NA ZA KUSISIMUA sehemu ya 1

Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 1 Uhakika media SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA Mwandishi: SEID BIN SALIM SEHEMU YA KWANZA Mwaka mmoja ukiwa umepita tokea binti mwenye umri wa miaka 24 lucky ajiunge na chuo kikuu cha dar es salam UNIVERSITY OF DAR ES SALAM. Marafiki zake aliokuwa anakaa nao chumba kimoja katika hostel waliojulikana kwa majina ya Mariam, Tunu, na amina. Asubuhi na mapema ya wiki end waliamua kumkalisha chini rafiki yao huyo kwa ajili ya kuongea nae mambo flan, kutokana na jinsi walivyokuwa wanaishi nae katika hali ya unyonge na kuonekana hapend kushirikiana na mtu yoyote kimasomo hd starehe za hapa na pale. waliishi nae kama sio mwenzao, walipoitaji ushirikiano wake hakuitaji kuwa nao, muda mwingine walimshuhudia akikaa kiupweke hadi kutoa machozi kwa muonekano wa kuwaza mambo mazito aliyonayo moyoni mwake, walimuonea huruma hasa kwa sababu wao ni watu waongeaji, walimkalia vikao vya kimya kimya walipopata nafasi ya kipeke ya...

NJIA 10 ZA KUTONGOZA KWA MACHO ZINAZO FANYA KAZI

Njia 10 za Kutongoza Kwa Macho Ambazo Hufanya Kazi Uhakika media   Je wataka kujifunza jinsi ya kutumia macho yako kupitisha ujumbe wa kuonyesha umevutiwa na mtu fulani? Kutumia macho kama mbinu ya kutongoza ni njia rahisi ya kupitisha ujumbe kutoka kwako hadi kwa yule unayemzimia kwa urahisi bila hata kutamka neno lolote. Mwanzo mchezo wa kutumia macho kama mbinu ya kutongoza huwa ina raha yake kiasi flani. Uzuri wa kutumia mbinu hii ni kuwa ni rahisi kufahamu kiwango gani mtu amevutiwa nawe bila kuwauliza kuwatoa out. Pili ni kuwa uzuri wa kutumia mbinu hii ni kuwa unamjulisha unayemzimia na mapema ya kuwa umewavutia hivyo kujitayarisha na mapema iwapo atakubali kufanya maongezi na wewe. So ni mbinu zipi hizo unazoweza kutumia kumvutia unayempenda bila kuonekana kama fala? Njia za kutongoza kwa kutumia macho Utafanya nini iwapo umemuona yule aliyekupendeza katika mkahawa ama katika party ulioalikwa na marafiki zako? Kama hujui la kufanya basi tumia macho yako kumtongoza...

Dawa 8 zinazo tibu kipanda uso kwa haraka

Uhakika media Dawa za asili 8 zinazotibu kipanda uso kwa haraka Dawa za asili 8 zinazotibu kipanda uso kwa haraka   Kipanda uso ni ugonjwa gani?   Kipanda uso ni maumivu ya kichwa ambapo kichwa kinagonga kweli kweli na mara nyingine inaweza kuwa sehemu ya mbele au upande mmoja wa kichwa ndiyo unapatwa na maumivu haya.   Maumivu haya yanaweza kubaki kwa saa 4 mpaka saa 72. Vile vile dalili za ugonjwa huu zinatofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine.   Dalili za Kipanda Uso:   Unaweza kupata baadhi ya ishara za ugonjwa huu kama vile; 1. Kujisikia uvivu, 2. Kutapika, 3. Mauzauza, 4. Kusikia kelele sikioni nk. Wakati mwingine kabla ya kipanda uso watu wengine wanaweza kupatwa na miwasho, shingo nzito, kupiga miayo, kusikia njaa nk Sababu za kutokea kipanda uso mara nyingi ni pamoja na: 1. Mfadhaiko wa akili (stress) 2. Kelele nyingi kuzidi 3. Kuluka kula mlo 4. Pombe 5. Siga...

Hatua za kufuata wakati wa tendo la ndoa

USIJE UMBUKA, SOMA HATUA ZA KUFUATA WAKATI WA KUFANYA MAPENZI....! Uhakika media Wapnzi na wanandoa wengi hivi leo wanapoingia kitandani tayari kwa kuianza safari ya kupeana haki zao za msingi hushindwa kufurahia tendo na hasa hali hii hujitokezwa kwa wanawake kwani mwanaume huwa na haraka iliyopitiliza!   Mwanaume atamkumbatia na kumbusu mwanamke kwa muda mfupi na kabla hata hamasa ya mapenzi ya mwanamke ahaijashika hatama, atamwingilia na ndani ya dakika sekunde ama dakika zisizozidi 3, mwanamme hufika mshindo. Katika hali ya kusikitisha baada ya mwanaume kujitosheleza hujongea pembeni bila kujali mwenza wake hajafika mwisho wa safari hali inayosababisha mwanamke kupoteza hamu ya tendo endapo endapo tabia hiyo ya mwanaume itaendelea. Kunahatua nne muhimu ambazo wapendanao wakizishika na kuzitekeleza ipasavyo basi watafanikiwa kujitosheleza kila wanapokutana na kwa hakika watakuwa miongoni mwa watu wachache wanaofurahia faragha kila wakutanapo! Hatua ya kwanza ni...

SIMULIZI NZURI NA YA KUSISIMUA sehemu ya 2

Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 2 uhakika media Riwaya: SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA. Mtunzi: SEID BIN SALIM SEHEMU YA PILI Ilipoishia... " hhhhhmmmmm. Aliguna tunu, kumbe na wewe umo?. Walinyanyuka na kicheko kila mmoja akabeba mkoba wake na kwenda darasani. lacky alitoka bafuni akiwa na khanga moja mwilini akakaa kitandani na kujifuta futa maji, hakukaa dakika akanyanyuka na kusogea kwenye kioo kujiangalia mwili wake wote ulivyo. Alivuta mafuta aina ya lotion akajipaka baadhi ya sehemu za mwili wake, alipomaliza aliitoa khanga mwili ukabaki utupu kisha akavaa nguo za ndani zilizokuwa kwenye henga.. Alimaliza kwa nguo za chuo akabeba mkoba na kutoka ndani, hadi anafika darasan hakuna alieweza kumpa hi kwa sababu ya kusikojulikana sana na watu, kwa alivyokuwa anajiweka hakuna aliweza kumzoea kwani hata mbinu ya kumuingia haikuwepo, wapo wanaume waliojifanya midomo mirefu kutaka kuingiza mistari ya kumtongoza kutokana na uzuri wa mvuto al...

SIMULIZI NZURI YENYE KUSISIMUA sehemu ya 3

Simulizi: SINA WA KUMLAUMU (Siitaji Kurudi Nilipotoka) Sehemu ya 3 Uhakika media Riwaya: SIITAJI KURUDI NLIKOTOKA. Mw/Mtunzi: SEID BIN SALIM SEHEMU YA 03 Ilipoishia...... " nimekuaribia usingizi wako ee, nsamehe mwaya! " wala, nlishaamka zamani wala usijali kuhusu hilo. " mapema yote hii. " yah kuna masomo jana yalinichanganya ndo nlikuwa nayapitia, si unajua asubuhi kunakuwa hakujachanganya masomo yanaingia?. " yah nalijua hilo, na wenzio vipi hao tayari au bado wameuchapa. Aliongea akiachia tabasam. " wao bado wamelala. " Ok poa, nakuomba ofisini kwangu mara moja basi nna maongezi na wewe samahani lakini. Alisema Sophia lucky akashangaa. Songa nayo...... " ofisini kwako? " Yah " um, kuna tatizo lolote? " Hapana lucky, ni mambo ya kawaida naitaji tuongee. " ok sawa nakuja. Alijibu akiwa na wasi wasi wa kuhisi uenda jamaa zake washapeleka malalamiko, Sophia alimuaga na kumuitaji asichelewe kisha akaondoka, l...

Hii ndio barua ya prof: Kitila Mkumbo kwenda kwa mkuu wa kanisa la KKKT

Hii ndio Barua ya Profesa Kitila Mkumbo Kwenda kwa Mkuu wa Kanisa la KKKT Uhakika media 5  · 1 hour ago Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) S. L. P. 3033 ARUSHA. Mheshimiwa Baba Askofu, Shalom!  YAH: MAMBO MATANO AMBAYO HAYAPONYI KATIKA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT   Jina langu ni Kitila Mkumbo, muumini katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambalo wewe ndiye mkuu wake. Kikazi, mimi ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Dodoma. Kitaaluma, mimi ni mhadhiri mwandamizi katika Saikolojia na Elimu nikiwa na cheo cha Profesa mshiriki katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.  Mheshimiwa Baba Askofu, kwa unyenyekevu mkubwa nimeamua kukuandika barua hii ili kutoa maoni yangu binafsi kwa kanisa unaloliongoza kupitia kwako kuhusu maudhui ya waraka uliotolewa na waheshimiwa maaskofu wa KKKT siku ya Jumamosi tarehe 24 Machi 2018. Waraka huo ulitarajiwa kusomwa katika makanisa siku ya Jumapili...

Misingi bora ya ufugaji wa mbuzi kibiashara

Misingi Bora Ya Ufugaji Wa Mbuzi Kibiashara Uhakika media · 20 minutes ago NAMNA BORA YA UFUGAJI.   1. Wafugwe kwenye banda bora.   2. Chagua kulingana na sifa zao na lengo la ufugaji (uzalishaji) nyama au maziwa.   3. Walishwe chakula sahihi kulingana na umri.   4. Kuzingatia ushauri wa mtaalamu wa mifugo hasahasa namna ya udhibiti wa magonjwa.   5. Kuweka kumbukumbu za uzalishaji.   6. Kuzalisha nyama au maziwa bora yanaokidhi mahitaji ya soko.   SIFA ZA ZIZI AU BANDA BORA LA MBUZI.   1. Banda bora linatakiwa liwe ni lenye kuweza kuwakinga mbuzi au kondoo na mashambulizi ya wanyama wakali (hatari) na wezi.   2. Liwepo sehemu ambayo maji hayawezi kutuama.   3. Mabanda yatenganishwe kulingana na umri.   4. Liwe na ukubwa ambao linaweza kufanyiwa usafi.   Kama utafuga mbuzi kwa kuwafungia (shadidi) muda wote zingatia yafuatayo:-   1. Banda imara lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya,upepo/mvua.   2. Lenye hewa ya...

Idara ya uhamiaji wafunguka kuhusu uraia wa Kidao

Idara ya Uhamiaji yafunguka kuhusiana na uraia wa Kidao Uhakika media 2  · 58 minutes ago Idara ya Uhamiaji nchini imesema inaendelea na uchunguzi juu ya uraia wa Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wilfred Kidao.  Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara hiyo, Ally Mtanda, amesema bado wapo kwenye uchunguzi na pale utakapokamilika watakuwa na majibu sahihi ya kusema.  "Bado tunaendelea na uchunguzi kuhusiana na suala hilo, pale utakapokamilika tutakuja na majibu sahihi ya kusema, kwa sasa bado haujakamilika" alisema Mtanda.  Hatua hiyo ilikuja mara baada ya kuelezwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu huyo hana uraia wa Tanzania.