Polisi nchini Kenya wameanza kufanya uchunguzi kuchunguza tukio la kifo cha mtoto wa umri wa miaka sita katika eneo la Suna nchini humo baada ya baba yake mzazi kumzika ardhini akiwa hai, hadi kupoteza maisha.
Inaelezwa kuwa usiku wa March 14, 2018 baba mtoto huyo anayejulikana kama Marcellus Odek alifika nyumbani hapo na kuchukua jembe kisha kuanza kuchimba shimo na baadaye kumchukua mtoto wake huyo na kuanza kumfukia.
Kwa mujibu wa Kiongozi Msaidizi wa eneo hilo Fredrick Owino, mwanaume huyo alifanya kitendo hicho kipindi ambacho hakukuwa na mtu yeyote nyumbani kasoro mke wake tu Annah Auma ambaye alimkuta amepoteza fahamu kutokana na ugonjwa wa kifafa ambao anao.
Owino amesema mwanaume huyo alipofika nyumbani alikuwa amelewa na hivyo alivyoyafanya kwa kiasi kikubwa yalishinikizwa na yeye kuwa amelala.
Maoni
Chapisha Maoni