Leo March 19, 2018 Rais John Magufuli ameeleza kuwa siku za hivi karibuni atakutana na Wakurugenzi Watendaji wawili kutoka nchi zaUjerumani na Demark ambao watakuja kufanya uwekezaji nchini.
Rais Magufuli ameeleza kuwa watakuja kufanya uwekezaji wa kiwanda kipya cha Petroli Kemikali (Petrol Chemical Plant) ambacho kitakuwa na thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1.92 ambayo ni sawa na takriban Shilingi za Kitanzania Trilioni 4.56.
Ameeleza kuwa kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira kwaWatanzania zaidi ya 4000 katika eneo la Kilwa kwaajili ya kutengeneza mbolea ambayo itauzwa ndani pamoja na nje ya nchi kwa kutumia gesi iliyopo nchini.
Maoni
Chapisha Maoni