KANUNI ZA KUANDAA KITALU CHA MBOGAMBOGA.
Uhakika media / 4 days ago
· Tengeneza tuta la kubwa wa 1m x 2m (ama urefu unaoona wewe kuwa unakufaaa ila tu upana ubaki kuwa 1mita) . Urefu na idadi ya matuta hutegemea kiasi cha
mbegu. Kiasi cha mbegu kwa hectare moja ni kilo 6 au 2 kg kwa eka.
mbegu. Kiasi cha mbegu kwa hectare moja ni kilo 6 au 2 kg kwa eka.
· Weka samadi iliyooza vizuri kiasi cha debe moja au mchanganyiko wa mbolea ya TSP na CAN (200gm) kwa uwiano wa 1:1 kwenye tuta changanya vizuri na udongo.
· Sia mbegu kwenye mistari kwa nafasi ya 1 sm x 20 sm. Tawanya mbegu vizuri wakati wa kusia ili miche isisongamane.
· Funika mbegu na weka matandazo ya nyasi kavu juu ya tuta na mwagiliwa maji. Udongo unatakiwa kuwa na unyevu kiasi mpaka mbegu ziote.
· Nyasi ziondolewe mara tu mbegu zikiota .
· Miche itunzwe vizuri na kitalu kiwe katika hali ya usafi.
· Miche imwagiliwe maji mpaka ifikie umri wa kupandikiza shambani.
· Sehemu ya kitalu iwe wazi, mbali na kivuli na kiwe karibu na chanzo cha maji.
KUMBUKA:siku za ukaaji wa mbegu kitaruni inategemeana na aina ya mbegu ama zao.
Maoni
Chapisha Maoni