Uhakika media· 3 hours ago
Na Ferdinand Shayo,Kilimanjaro
Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro Dr.Stanley Hotay ameitaka serikali kutobadili sera ya elimu mara kwa mara ili kudhibiti kiwangocha elimu pamoja na kuondoa mikanganyiko inayojitokeza kufuatia mabadiliko hayo.
Askofu Dk. Hotay ametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa shule ya sekondari bishop alpha memorial high school inayomilikiwa na kanisa hilo anasema mabadiliko ya sera ya elimu yamekua yakiwachanganya wadau wa elimu hivyo ni vyema sera hizo zikaa kwa muda badala kubadilika katika kila awamu ya uongozi.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha anasema serikali itaangalia uwezekano wa kushughulikia changamoto za kisera zilizoanishwa na wadau wa elimu .
Nasha amesema kuwa serikali inatambua mchango wa taasisi za dini katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu na afya jambo ambalo linasaidia kuwahudumia Watanzania hivyo wataendelea kushirikiana na taasisi hizo.
Akizungumza katika tukio ilo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi amesema wamiliki wa shule wanalojukumu kuisaidia serikali kwa kutoa elimu bora yenye maadili na nidhamu .

Maoni
Chapisha Maoni