Dawa mbadala 10 zinazotibu shinikizo la chini la damu
Published by fadhili on 08/09/2017

Shinikizo la chini la damu hujulikana pia kama hypotension kwa Kiingereza. Ni hali ambayo shinikizo la damu ya mtu linakuwa chini sana na kusababisha dalili kama kizunguzungu, uchovu, udhaifu, kupumua kwa shida, kupungua kwa nuru ya macho nk
Utaambiwa una shinikizo la kawaida la damu kama vipimo vitasoma una 120/80 mm Hg.
Hata hivyo ikiwa vipimo vitasoma una
90/60 mm Hg au chini ya hapa, utaambiwa una shinikizo la chini la damu. Shinikizo la damu linapokuwa chini zaidi linaweza kupelekea msukumo ulio chini wa damu kwenye ogani kama ubongo, figo, na kwenye moyo.
Tatizo hili linaweza kusababishwa na vitu kama kupungua kwa maji mwilini, kulala sana, lishe duni, kushuka kwa wingi wa damu, matatizo ya moyo, ujauzito, homoni kutokuwa sawa na kadharika.
Baadhi ya dawa za hospitalini pia zinaweza kusababisha tatizo hili.
Unaposhughulika na shinikizo la chini la damu inashauriwa kuongeza matumizi ya chumvi na maji. Hata hivyo wasiliana na daktari wako wa karibu kabla kuamua lolote mwenyewe binafsi.
Kupona kabisa kwa tatizo hili kunategemea na aina hasa ya chanzo chake, hata hivyo unaweza kujaribu dawa mbadala zifuatazo ili kuzuia, kutibu au kupunguza dalili zake.
1. Maji chumvi
Maji yenye chumvi husaidia kutibu shinikizo la chini la damu sababu sodiamu iliyomo kwenye chumvi hupandisha juu shinikizo la damu. Usizidishe dawa hii hata hivyo sababu chumvi nyingi kuzidi ina madhara kiafya.
Matumizi: Changanya nusu kijiko cha chai cha chumvi ndani ya maji glasi moja (robo lita) na unywe mchanganyiko huu mara 1 au 2 kwa siku
2. Kahawa
Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kunaweza pia kusaidia kupandisha shinikizo lako la damu kwa muda. Kama unapatwa na kushuka kwa shinikizo la damu mara kwa mara basi kunywa kikombe cha kahawa asubuhi au unywe wakati unakula cha mchana na cha jioni.
Hata hivyo usizidishe matumizi ya kahawa kwakuwa kahawa ina madhara mabaya kwa afya ya mwili kwa ujumla.
Vitu vingine ambavyo ni sawa na kahawa ni pamoja na cocoa, chai ya rangi, energy drinks zote, na soda nyeusi zote. Kuwa makini hata hivyo utumiavyo vitu hivi vikizidi vina madhara mwilini.
3. Zabibu kavu
Zabibu ni dawa ya asili inayotumika sana katika tiba za asili za India kutibu shinikizo la chini la damu kwa namna ya asili kabisa.
1. Loweka zabibu 30 mpaka 40 ndani ya kikombe cha maji kwa usiku mzima.
2. Asubuhi kabla ya kula wala kunywa chochote kula hizo zabibu moja baada ya nyingine na unywe pia maji yake
3. Fanya zoezi hili kila siku kwa majuma kadhaa hata mwezi.
4. Mrehani
Mrehani (basil) ni dawa nzuri ya kutibu shinikizo la chini la damu sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C, magnesiamu na potasiamu, pia inasaidia kuweka sawa akili na kuondoa msongo wa mawazo (stress).
1. Chukua majani 10 mpaka 15 ya mrehani mbichi (freshi) na usage au utwange upate maji maji yake (juisi).
2. Ongeza asali kijiko kidogo kimoja ndani yake.
3. Kunywa mchanganyiko huu kila siku asubuhi ukiamka tu tumbo likiwa tupu.
Unaweza pia kuwa unatafuna tu moja kwa moja majani kadhaa ya mrehani kila siku asubuhi.
5. Lozi na maziwa
Hii ni dawa nyingine ya asili kwa ajili ya shinikizo la chini la damu.
1. Ziloweke lozi 5 mpaka 6 kwenye kikombe cha maji kwa usiku mmoja.
2. Asubuhi menya hizo lozi na uzisage.
3. Chukua hizo lozi ulizosaga na uweke ndani ya kikombe cha maziwa na uchemshe kwa dakika kadhaa. Kunywa kinywaji hiki kila siku asubuhi.
6. Juisi ya karoti na asali
Kuanza siku yako na juisi freshi ya karoti iliyochanganywa na asali ni njia rahisi ya kutibu shinikizo la chini la damu.
1. Chukua glasi moja ya juisi ya karoti
2. Ongeza vijiko vikubwa viwili vya asali ndani yake
3. Changanya vizuri na unywe yote asubuhi tumbo likiwa tupu na jioni glasi nyingine kwa majuma kadhaa
7. Juisi ya limau
Juisi ya limau ni nzuri sana katika kutibu shinikizo la juu la damu, lakini inaweza pia kutumika kutibu shinikizo la chini la damu hasa ikiwa hili shinikizo la chini la damu limesababishwa na upungufu wa maji mwilini (dehydration).
Katika kutibu shinikizo la chini la damu unaweza kuchanganya juisi ya limau (maji maji ya limau) na chumvi kidogo na sukari. Hii inasaidia kuupa nguvu mwili wako kwa kuhamasisha utendaji kazi wa ini na kusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
Unaweza pia kuchukua juisi ya miwa ukiongeza maji maji ya limau kijiko kidogo kimoja na chumvi kidogo kwa ajili hii.
8. Tangawizi
Tangawizi ni dawa maarufu imekuwa ikitumika kutibu shinikizo la juu la damu pia shinikizo la chini la damu. Tangawizi ina vitu vingi mhimu ndani yake ikijumuisha viuavijasumu sambamba na kemikali mimea zenye nguvu sana kama ‘gingerol’, ‘shogaol’, na ‘zingerone’, ambazo zinaweza kusaidia kuwa sawa msukumo wa damu.
Kazi kubwa hasa ya tangawizi ni kuwa huifanya damu isigande kazi ambayo ni mhimu katika kuweka sawa shinikizo la damu.
Unahitaji:
Kijiko kikubwa kikubwa cha tangawizi mbichi iliyoparuzwa (grated)
Kikombe kimoja cha maji ya moto
Chemsha katika moto kwa dakika 12 hivi
Kisha ipua na uchuje
Ikipoa kidogo kunywa yote, fanya hivi mara 2 kwa siku kila siku
9. Maji ya kunywa
Hii ni moja ya dawa rahisi kabisa ya shinikizo la chini la damu. Maji ni mhimu kwa kila ogani ndani ya mwili iweze kufanya kazi zake sawa. Hivyo sababu kuu ya mtu kuwa na shinikizo la chini au hata la juu ni matokeo ya mishipa ya damu kutokuwa na vimiminika vya kutosha.
Kwa ujumla mishipa yako ya damu imeundwa kwa maji maji ya damu (serum) na seli za damu. Ile ukijikata unaona damu inatoka hivi yale huwa ni maji ambayo ndani yake ndiyo kuna seli za damu (blood cells).
Muda wowote maji yanapopungua kwenye mwili wako hata vipenyo vya mishipa yako navyo hupungua ukubwa wake jambo linaloleta kushuka kwa shinikizo la damu. Matatizo yote haya ni matokeo ya kutokunywa maji ya kutosha kila siku.
Kwahiyo ili kupandisha juu shinikizo la damu unahitaji kunywa zaidi maji sambamba na juisi nyingine za matunda au za mboga mboga kila siku.
10. Kupangilia chakula
Pamoja na kutumia dawa mbadala 9 hapo juu, bado unahitaji kuwa bize na mazoezi ya viungo kila siku ili kuhamasisha mzunguko mzuri wa damu. Epuka mazoezi mazito na ya kunyanyua vyuma vizito sana.
Wasiliana pia na daktari wako ikiwa dawa zozote unazotumia za ugonjwa wowote sasa zinaweza kuwa zinasababisha shinikizo la chini la damu au la.
Pia ni mhimu kula mlo kamili kila siku. Kula lishe duni kunaweza kupelekea kuzalishwa kwa damu isiyo na afya inayoleta shinikizo la damu.
Upungufu wa baadhi ya vitamini hasa vitamini za kundi B na madini kunaweza pia kuleta shinikizo la chini la damu. Hivyo ili kudhibiti shinikizo la chini la damu unahitaji kula mlo sahihi kila siku.
Kula zaidi vyakula vyenye protini, vyenye vitamini B na C kwa wingi. Kula milo midogo midogo hata mitano kuliko kula miwili au mitatu lakini ya nguvu sana.
Acha vilevi vyovyote mara tu unapogundulika na shinikizo la chini la damu. Epuka pia vyakula vyenye wanga sana kama tambi, mikate, viazi, wali nk
Pendelea pia kutumia kitunguu swaumu hasa kibichi ukitafuna punje 2 kila unapoenda kulala kadharika glasi moja ya juisi ya ubuyu kutwa mara 1.
Kwa mawasiliano zaidi: WhatsApp +255769142586

Maoni
Chapisha Maoni