Jitibu aleji kwa kutumia Binzari
Published by fadhili on 27/08/2017
Jitibu aleji kwa kutumia Binzari
Je unatafuta dawa ya asili nzuri na yenye uhakika ya kutibu aleji? Umechoka kutumia dawa zenye kemikali zinazokuacha na madhara mengine baada ya kuzitumia?
Kama ni ndiyo basi manjano inaweza kuwa mbadala mzuri wa kuuendea ili kujitibu na aleji.
Ni mhimu kwamba unafanikiwa kujitibu aleji mapema kabla haijawa sugu. Hata hivyo manjano au binzari ni dawa nzuri ya asili kwa kutibu aleji.
Unahitaji kufahamu zaidi namna inavyofanya kazi? Endelea kusoma
Jitibu aleji kwa kutumia manjano:
Labda kama una aleji tena na binzari, kinyume na hapo unatakiwa utumie kama dawa yako mbadala ya kukutibu aleji. Ni dawa yenye nguvu ya asili ya kutibu aleji sababu ina vitu vinavyoweza kudhibiti dalili mbalimbali za aleji.
Namna ya kutumia binzari kujitibu na aleji:
1. Manjano ina kitu kinaitwa ‘curcumin’ ambacho ndicho kinahusika katika kudhibiti dalili mbalimbali za aleji
2. Kiungo hiki manjano kinafanya kazi kama mdhibiti wa asili wa histamini (natural antihistamine). Hii inamaanisha binzari inao uwezo mahususi wa kuzuia kutolewa kwa histamini katika mwili wako na hivyo kuzuia dalili na ishara za aleji.
3. Binzari ni mdhibiti mzuri dhidi ya maambukizi mbalimbali, dhidi ya bakteria, na hivi vyote kwa pamoja vinasaidia kuondoa dalili za aleji.
4. Binzari inaweza kuongeza kinga ya mwili ambayo huwa inapotea kama matokeo ya dalili za aleji.
5. Binzari kwa asili kabisa inaweza kuzuia kuongezeka kwa ‘leukotriene’. Leukotriene inahusiana na aina fulani za aleji kama pumu ya koo na matatizo mengine mengine mapafu.
6. Binzari inaweza kutumika kutibu aleji zote ile aleji sugu na hata aleji ya kawaida. Unahitaji tu uitumie kwa kipindi kirefu mpaka umeanza kuona unapona. Matumizi ya mara kwa mara ya kiungo hiki hayana madhara na unaweza kuitumia kwenye vyakula vyako vingi kama kiungo.
Soma pia hii > Jitibu Aleji (Allergy) kwa kutumia Maji ya Kunywa
Namna ya kutumia binzari kujitibu aleji:
Kama nilivyosema hapo juu unaweza kuitumia binzari kwenye vyakula vyako vingi unavyopika kila siku. Kuna namna nyingine kadhaa unaweza kuitumia:
Njia ya kwanza:
Unahitaji: Binzari ya unga nusu kijiko kidogo kimoja cha chai, maziwa ya moto kikombe kimoja, asali na pilipili manga nyeusi ya unga.
Changanya hivyo vyote pamoja. Kunywa mchanganyiko huu kutwa mara 2 au 3 kwa siku. Kama utakunywa asubuhi basi kunywa tumbo likiwa tupu kabla hujala wala kunywa chochote.
Njia ya pili:
Changanya nusu kijiko cha chai ya binzari cha unga na maji ya uvuguvugu kikombe kimoja, Ongeza asali kidogo kupata radha. Kunywa mchanganyiko huu kutwa mara 2 kila siku mpaka umepona.
Unaweza kutumia binzari au manjano kama dawa yako ya nguvu mbadala ya kujitibu aina mbalimbali za aleji. Ni dawa salama na inaweza kutumika kwa namna nyingi mbalimbali.
Hivyo wakati mwingine ukipata aleji usikimbilie duka la madawa, nenda tu jikoni kwako chukua binzari na uendelee na matibabu na ushuhudie maajabu haya bila gharama yoyote.
Ni matumaini yangu makala hii imekusaidia, nipe mrejesho wa hali yako baada ya kuijaribu dawa hii kupitia comment hapo chini.
Kuna dawa nyingine ya asili umeitumia kujitibu aleji na umepona? Kama ndiyo nitajie hapo chini na mimi niendelee kujifunza.
Kama utahitaji Binzari niachie ujumbe WhatsApp +255769142586
Tafadhali SHARE kwa ajili ya wengine.

Maoni
Chapisha Maoni